Wednesday, 17 February 2016

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni ameiomba Ujerumani

 iinasihi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ikubali kubadilishana mateka wa Kipalestina kwa viwiliwili vya wanajeshi wawili wa utawala wa Kizayuni vilivyoko mikononi mwa Hamas.
Mtandao wa habari wa Palestine Today umemnukuu Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Kizayuni akiliambia gaeti moja la Israel kuwa, viongozi wa Ujerumaini wamekubali kuwa wapatanishi katika suala zima la kubadilishana na Hamas, mateka wa Kipalestina kwa viwiliwili vya wanajeshi wawili wa Israel.
Amesema, katika miaka ya huko nyuma pia Ujerumaini iliwahi kuisaidia Israel katika suala kama hilo, hivyo hivi sasa anaiomba tena iusaidie utawala wa Kizayuni.
Wanamapambano wa Palestina waliwateka nyara wanajeshi hao vamizi wa Israel wakati walipouvamia Ukanda wa Ghaza katika mashambulizi ya siku 50 yaliyoanzishwa na Israel dhidi ya ukanda huo uliozingirwa kila mahali.

Thursday, 11 February 2016

Mburu
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina Geoffrey Mburu ambae anajiusisha mapenzi ya jinsia moja amejisalimisha mikononi mwa polisi kutokana na kutafutwa kwa kosa la kumtumia ujumbe wa maandishi mtangaza na mwandishi wa kituo cha radio, mtangazaji uyo aliyejulikana kwa jina la Victor Kinuthia ambae anafanya kwenye kampuni ya Royal Media Services. Kijana uyo alipo tuma ujumbe wa maandishi ndipo kiruthi alipoamua kumfungia ili asitume tena ujumbe wa maandishi, lakini Mburu alipoona ujumbe auendi wa maandishi ndipo alipo tuma ujumbe wa sauti uliopelekea mwandishi uyo kwenda kutoa taarifa polisi, mtuhumiwa lipojisalimisha na kufikishwa katika kituo cha polisi Murang’a alikili na ndipo alipo takiwa kulipa faini

Wednesday, 20 January 2016

Umoja wa Mataifa umetaka kutolewa msaada wa zaidi ya dola bilioni moja kwa ajili ya Sudan.
Eugene Owusu, Mratibu wa oparesheni za misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jumanne wiki hii amesema kuwa kwa uchache msaada wa fedha wa dola bilioni moja na laki tatu unahitajika kwa ajili ya kuwasaidia raia zaidi ya milioni tano wa Sudan Kusini ambao wanakabiliwa na hali ngumu. Owusu ameongeza kuwa katika kila watu kumi nchini Sudan Kusini, watu wawili walizikimbia nyumba zao miaka miwili iliyopita kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapigano kati ya serikali ya waasi wa nchi hiyo. Mratibu wa oparesheni za misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesisitiza kuwa umoja huo unakabiliwa na changamoto kubwa nchini humo.
Watu zaidi ya elfu kumi wameuliwa na wengine zaidi ya milioni mbili na laki tatu wamekuwa wakimbizi tangu kuzuka mapigano huko Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka 2013
sos Thran

Monday, 11 January 2016



Najua uliwai kujiuliza maswali mengi na kuhusu ukimya wa Ali Kiba mala tu baada ya
kutoa ngoma yake ya Chekecha cheketea sasa majibu ni sipo tu kwani kwa sasa
wamefanya ngoma ya pamoja na Christian Bella mzigo ndio uo kama ulivyouangalia apo juu

Saturday, 19 December 2015

 Kama ulizani ni Tanzania pekee ndio inatumia wasanii wake kwenye kipindi cha Uchaguzi basi ni sio pekee kwani hata Uganda nao wameendelea kuwatumia wasanii wakubwa
 Picha ni Bebe Cool akiwa kwenye kampeni sambamba na msanii wa kundi la Goodlyfe ambae pia ni mdogo wake na Jose Chameleon
Kampeni izo ni za kumnadi mgombea wa kiti cha uraisi kupitia chama cha NRM ambae mgombea wake ni Raisi Mseveni ambae kwa sasa ndie raisi wa Uganda na Bebe Cool amemmwagia sifa nyingi tu mala baada ya kampeni kwisha alisema haya

And this was the day today in Tororo district.
This is to comfirm to you my fellow Ugandans that monitor publication findings where right.
The old man is still loved for the people who appreciate the little they have in this peaceful UGANDA.

Friday, 4 December 2015

 Simba akiwa kwenye doria yake ya kusaka chochote kitu mala tu baada ya kuona kwa mbali grupu la wanyama aina ya nyumbu wakiwa kwenye msafara wao kwa wale waliowai kutembelea mikumi nadhani watakuwa wanajua ni jinsi gani wanyama hawa wanavyotembea kwa makundi
 Kwa bahati mzuri simba alifanikiwa kutege mtego wake wa kukaa pembeni mwa njia wanaoitumia kupita wanyama hao kuelekea mtoni na maeneo hayo ayo ndio watalii na wawindani upendelea kwenda kuwinda na kupiga picha au kujionea wanyama na tabia zao japo kwa muda mfupi tu

 Simba wa kwanza kati yao alianza kwa kuingia msafara uo na kufanikisha kuwatawanya ndipo walipofanikiwa pia kubaki na Nyumbu wawili ambao walianza kuwashughulikiwa, wakati zogo ilo likiendelea watalii na wawindani walianza kwa kuwashangaa na kupiga picha nyingi sana uku wakiwaangalia kwa umakini kwa lengo la kutaka kujua kama simba ataendela kuwa mshindi siku zote kwa kila ananchokitaka,

Baada ya piga nikupige ya muda mrefu atimae Nyumbu walifanikiwa kuwazidi akili simba na kufanya simba watafute mbadala mungine wa chakula ambao jirani tu kuliwa na mzoga aikuthibitishwa kama ulikuwa umeharibika au ni mzima ila simba jike ao walianza kuushambulia vizuri

Mala nyingi simba dume upendelea sana kula kile ambacho amekiwinda mwenyewe tofauti na simba jike ambae mala kadhaa amezoea kuletewa chakula ndio maana aikuwa ajabu kuona wanakula mizoga

Wednesday, 18 November 2015

Baraza la seneti nchini Rwanda limepitisha mabadiliko mapya ya kipengele cha katiba kitakachomruhusu Rais Paul kagame kuendelea kubaki madarakani hadi mwaka 2034.

Uwamuzi huo ulichukuliwa kwa sauti moja siku ya Alhamis. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatafikishwa mbele ya wananchi ili kuweza kupiga  kura ya maoni ambayo inatarajiwa kupata ushindi kiurahisi.
Rais Kagame mwenye umri wa miaka 58, ameiongoza nchi ya Rwanda tangu jeshi lake lilipomaliza mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 na kuwaondoa madarakani wahutu wenye msimamo mkali nchini humo. Chini ya sheria iliyopo hivi sasa, bwana Kagame anatakiwa kujiuzulu mwishoni mwa muhula wake wa pili madarakani mwaka 2017.

Lakini kipengele kilichopendekezwa kinamruhusu bwana Kagame kuwania muhula mwingine wa miaka saba madarakani, kisha ikifuatiwa na mihula miwili ya miaka mitano madarakani.
Chanzo: VOA Swahili

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS