Umoja wa Mataifa umetaka kutolewa msaada wa zaidi ya dola bilioni moja kwa ajili ya Sudan.
Eugene Owusu, Mratibu wa oparesheni za misaada ya kibinadamu wa
Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jumanne wiki hii amesema kuwa kwa
uchache msaada wa fedha wa dola bilioni moja na laki tatu unahitajika
kwa ajili ya kuwasaidia raia zaidi ya milioni tano wa Sudan Kusini
ambao wanakabiliwa na hali ngumu. Owusu ameongeza kuwa katika kila watu
kumi nchini Sudan Kusini, watu wawili walizikimbia nyumba zao miaka
miwili iliyopita kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na mapigano
kati ya serikali ya waasi wa nchi hiyo. Mratibu wa oparesheni za misaada
ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesisitiza kuwa
umoja huo unakabiliwa na changamoto kubwa nchini humo.
Watu zaidi ya elfu kumi wameuliwa na wengine zaidi ya milioni mbili na laki tatu wamekuwa wakimbizi tangu kuzuka mapigano huko Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka 2013
sos Thran
Watu zaidi ya elfu kumi wameuliwa na wengine zaidi ya milioni mbili na laki tatu wamekuwa wakimbizi tangu kuzuka mapigano huko Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka 2013
sos Thran
0 comments:
Post a Comment