millanzy Pages
Mahakama Kuu ya Rwanda imemsafishia njia Rais Paul Kagame wa nchi hiyo ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula mwingine wa miaka saba, baada ya kutupilia mbali kesi ya kuzuia marekebisho ya katiba
iliyokuwa imewasilishwa na chama kikuu cha upinzani.
Mahakama hiyo imesema katika taarifa yake kwamba, kesi iliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Democratic Green Party of Rwanda haikuwa na maana yoyote. Chama hicho kilitaka kulizuia Bunge kubadilisha kipengee cha katiba nambari 101 kinachoweka ukomo wa Rais kugombea kiti cha Urais wa zaidi ya mara mbili. Jaji Mkuu Sam Rugege amesema katika uamuzi wake katika mahakama hiyo mjini Kigali kwamba, mahakama imegundua kuwa kipengee nambari 193 cha katiba hiyo kinaruhusu kipengee 101 kubadilishwa iwapo hilo litafanywa na wananchi kupitia kura ya maoni. Hata hivyo kiongozi wa Democratic Green Party of Rwanda, Frank Habineza amewaambia waandishi habari kuwa walitarajia kushinda keshi hiyo lakini mahakama imewavunja moyo.
Zaidi ya watu milioni 3.7 sawa na zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura walitia saini ombi la kutaka mabadiliko ya katiba ili kumruhusu Rais Kagame kugombea kwa muhula mwingine katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017
join facebook Page

0 comments:
Post a Comment