Thursday, 14 May 2015

rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, katikati, akisindikizwa katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, jinini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 13, 2015.

Hali nchini Burundi inazidi kuwa kitendawili huku kukiwa na taarifa zenye kutatanisha kutoka pande zinazopingana nchini humo.
Kundi linalompinga rais  Pierre Nkurunziza linadai kushikilia maeneo muhimu nchini humo huku taarifa kutoka kwa serikali ikisema kuwa bado serikali iko thabiti  chini ya uongozi wa Rais Nkrunziza.
Hata hivyo hali ya taharuki inaendelea kutanda kote nchini humo, huku raia wasijue cha kutarajia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa  Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika,mjini Bujumbura,  Haidalla Hakizimana, milio ya risasi na milipuko imesikika usiku kucha na kufikia asubuhi ya Alhamisi.
Inasemekana kuwa radio binafsi zilikuwa zimeshambuliwa na wanaodaiwa kumuunga mkono rais Nkurunziza.
Raia walibaki majumbani kwa hofu ya kushambuliwa na kukosa uhakika wa nani mwenye mamlaka katika nchi kwa sasa.
Shughuli za kawaida kama usafiri zimekatizwa na wala hakuna watoto wanao hudhuria masomo hasa kwenye mji mkuu Bujumbura.
Wakati huohuo mwenyekiti wa chama cha madereva wa magari makubwa Tanzania, Clement Masanja amesema kuna magari kadhaa makubwa pamoja na madereva  wamekwama nchini Burundi kufuatia matatizo haya ya kisiasa.
Anasema  chama chake kimelazimika kusimamisha kwa muda usafirishaji mizigo kwenda  nchini Burundi mpaka hali itakapokuwa nzuri.
Ameongezea kuwa chama chake kinafanya juhudi za kuwasiliana na mamlaka husika nchini Burundi kubuni njia za kuwarudisha nyumbani  madereva wliokwama nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS