Sunday, 12 April 2015


 Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametaka Wapalestina wote wauawe. Shirika la habari la Palestina limemnukuu Avigdor Lieberman akisema hayo leo na kuongeza kuwa, hatarejea kwenye Baraza la Mawaziri la serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, hadi pale Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itakapofutwa kikamilifu na wanachama wake wote kuuawa. Lieberman ambaye ni mkuu wa chama cha Yisrail Beiteuni pia amemlaumu Benjamin Netanyahu kwa kukwepa mazungumzo ya muungano unaounda serikali ya utawala wa Kizayuni katika kuunda Baraza la Mawaziri. Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa bunge la utawala wa Kizayuni "Kneset" wa tarehe 17 mwezi uliopita wa Machi, chama cha Likud kilipata viti 30, muungano unaojulikana kwa jina la "Umoja wa Kizayuni" ulipata viti 24 na muungano wa vyama vya Waarabu ukapata viti 13 kati ya viti 120 vya bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Israel, Baraza la Mawaziri linaundwa na chama kikuu lakini kiongozi wa kila chama atakayeweza kuunda muungano wenye viti vingi zaidi bungeni, hupewa yeye jukumu la kuunda serikali na Baraza la Mawaziri.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS