![watu 9 wauliwa katika machafuko ya uchaguzi Nigeria](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_scRPbr7x5aT684p8JLDWy06jwgYHcbnMa4WCjYyQu0JwL-6bGY3RdXeKW83-hx8nFJm3fj8tKtCKLgq_ggl9RF5OMF0v0ghc5jjs3FGIniqOlTWIR3uESfhgFFxv1uk7QX2Rv1f_F-8gQrzqDEkFAPzdS-iU9lWg=s0-d)
Watu tisa wameuawa kwenye ghasia na maandamano huko kusini mwa Nigeria,
wakati nchi hiyo ikiwa imeendesha chaguzi za magavana wa majimbo.
Machafuko hayo yaliripotiwa jana, ambapo mengi yalishuhudiwa katika
jimbo la Rivers ambalo ni tajiri kwa mafuta. Dakuku Peterside mgombea wa
upinzani kutoka chama cha APC amesema kuwa wafuasi wake wanane
wameuawa, huku duru za polisi zikisema kuwa afisa mmoja pia amepoteza
maisha kwenye ghasia hizo. Ripoti zinasema kuwa, ufyatuaji risasi
ulisikika pia katika miji kadhaa katika jimbo la Rivers. Kituo cha
kupigia kura na nyumba ya Manuela George-Izunwa, Kamishna wa jimbo la
Rivers anayehusika na masuala ya wanawake vimechomwa moto pia. Mawakala
wa uchaguzi karibu kumi walitekwa nyara mapema jana huku maelfu ya
waandamanaji huko Port Harcourt makao makuu ya jimbo la Rivers,
wakiichelewesha kufunguliwa vituo vya kupigia kura.
0 comments:
Post a Comment