Mwanafunzi mmoja wa Mkenya ameaga dunia na wengine zaidi ya 100
kujeruhiwa wakati wakikimbia, baada ya transfoma ya umeme kuripuka
katika bweni moja la wanachuo katika Chuo Kikuu cha Nairobi kabla ya
alfajiri ya leo. Mripuko huo uliibua wasiwasi na wahaka katika mabweni
ya wanachuo wakidhani kuwa wamevamiwa. Katika tuki hilo lililotokea
mapema leo, baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi waliruka
madirishani ili kujinusuru, ikiwa zimepita siku chache tu baada ya
wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab kukishambulia Chuo Kikuu cha
Garissa na kuuwa wanafunzi zaidi ya 100. Peter Mbithi, Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Nairobi amesema kuwa, mwanafunzi aliyefariki dunia
alikuwa kati ya wale walioruka kutoka kwenye bweni lao lililoko katika
ghorofa tano, wakihofia majengo ya chuo hicho yamevamiwa. Walioshuhudia
mripuko huo wa transfoma ya umeme wamesema kuwa iliripuka saa 10.30
alfajiri ya leo kwa saa za Kenya na hivyo kusababisha wanafunzi wa kike
kuanza kupiga kelele na hofu hiyo kuenea pia kwa upande wa wavulana, na
kisha wanafunzi wakaamka na kuanza kujaribu kutoka nje.
Sunday, 12 April 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment