Tuesday, 3 March 2015

 

Maelfu ya wanawake katika Jamhuri ya Congo Brazzaville wameandamana wakilalamikia mivutano ya kisiasa katika nchi yao. Maandamano hayo makubwa yamefanyika katika mji mkuu Brazzaville. Waandamanaji hao wametoa wito wa kuweko amani na uthabiti wa kisiasa katika nchi yao. Wanawake wa Jamhuri ya Congo Brazzaville wamefanya maanadamo hayo wakitaka kuweko utulivu wa kisiasa katika nchi yao baada ya kutokea mvutano na mzozano baina ya serikali ya nchi hiyo na vyama vya upinzani. Mvutano baina ya serikali ya Congo Brazzaville na vyama vya upinzani umeshadidi baada ya pande mbili kutofautiana kuhusiana na marekebisho ya katiba ya nchi hiyo. Uchaguzi wa Jamhuri ya Congo Brazzavile umepangwa kufanyika mwaka ujao. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, ukomo wa uongozi wa Rais ni duru mbili tu na Rais wa nchi hapaswi kuwa na zaidi ya miaka sabini. Agosti mwaka ujao Rais Denis Sassou Nguesso anakamilisha duru mbili za uongozi hivyo kwa mujibu wa katiba ya nchi hapaswi kugombea katika uchaguzi ujao


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS