Tuesday, 3 March 2015

Raisi Jakaya Kikwete akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa mwito wa kusakwa na kutiwa mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya albino nchini humo. Rais Jakaya Kikwete amezungumzia hali ya usalama wa nchi, ikiwemo uvamizi wa vituo vya polisi, uporaji wa silaha ulioambatana na vifo vya askari na kusema, matukio hayo, baadhi yake yana dalili za ugaidi. Akizungumzia hali ya usalama nchini humo katika hotuba yake ya mwishomi mwa mwezi Februari, Rais Kikwete pia amekemea vikali vitendo vya mauaji dhidi albino na kubainisha kwamba, vitendo hivyo vinafedhehesha, kudhalilisha taifa na kwamba, katu havivumiliki. Rais Kikwete amekubali kukutana na viongozi na wanachama wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi, kwa lengo la kuwasikiliza na kuangalia jinsi ya kumaliza mauaji ya watu hao, yanayofanywa kwa imani ya ushirikina. Rais Kikwete amesema: "Nimesikitika na mauaji ya ndugu zetu albino. Ni vitendo vya kinyama ambavyo havitegemewi kufanywa au kutokea katika jamii yeyote. Naamini ushirikiano wa karibu kati ya serikali na jamii utatuwezesha kutokomeza mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi na kuliondolea taifa letu aibu hii".


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS