Tuesday, 3 March 2015

Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, atalihutubia Bunge la Marekani Jumanne katika hotuba inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Awali, Netanyahu alisema  Marekani, na Israel, zinakubaliana kwamba kuna haja ya kuizuia Iran kuwa na silaha za nyuklia lakini hazikubaliani namna ya kufikia lengo hilo.

Kauli hiyo ilitolewa siku moja kabla ya waziri mkuu huyo kuhutubia bunge la Marekani.

Mwaliko wa kulihutubiua  Bunge umezusha utata Marekani kwa sababu unafanyika  bila ya utamaduni wa kawaida wa kushauriana na White House.

Hatua hiyo imeonyesha mvutano wa uhusiano uliopo baina ya bwana Netanyahu, na rais wa Marekani, Barack Obama.

Bwana Netanyahu anasema kutokukubaliana na Marekani, kunatokana na mitazamo tofauti kwa sababu Washington, inawasiwasi na usalama wakati Israel inahofu na uhai.

Katika mahojiano na shirika la habarfi la Reuters, bwana Obama amesema utawala wake na serikali ya Israel unatofautiana kwa namna ya kuiwezesha Iran kutokuwa na nguvu za nyuklia.


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS