Tuesday, 3 March 2015

Bunge la Libya, lililochaguliwa na wananchi  limekubali kurudi katika majadiliano ya amani yanayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hii ni wiki moja baada ya kujitoa na mjumbe wa Bunge linalohasimiana  kusema mazungumzo yanatarajiwa kuanza siku ya Alhamisi.

Mataifa ya magharibi yanaona mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kama nafasi pekee ya kumaliza mzozo wa Libya wa kugombania madaraka kati ya serekali mbili pinzani na majeshi yao.

Hali ya kutoelewana inaweza kuhatarisha kuipeleka nchi hiyo katika vita zaidi  ya wenyewe kwa wenyewe inayokaribia miaka minne sasa tangu kuondolewa kwa utawala wa Muammar Gaddafi.

Wakati huo huo, Khalifa Haftar, kiongozi muhimu katika mapinduzi ya Libya amechaguliwa kuwa mkuu wa jeshi la serikali inayotambulika kimataifa.

Uteuzi wa Haftar unaonekana unaweza kuleta taharuki katika mazungumzo  hayo ya Umoja wa Mataifa ya kujaribu  kumaliza mzozo wa nchi hiyo


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS