Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amemfukuza kazi makamu wake,
Samuel Sam-Sumana kutokana na kuomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani
mjini Freetown.
Taarifa iliyotolewa na Rais Koroma imesema Sam-Sumana ameacha majukumu yake na ofisi ya Makamu wa Rais na kwamba atateua Makamu mpya wa Rais.
Kwa upande wake Sam-Sumana amesema ameshtushwa na uamuzi huo wa Rais Koroma na kwamba unakiuka katiba ya nchi hiyo. Amesisitiza kuwa Rais Koroma hana mamlaka ya kumfuta kazi Makamu wa Rais na kwamba atawasilisha mashtaka dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama Kuu ya Sierra Leone.
Makamu wa Rais wa Sierra Leone aliomba hifadhi katika ubalozi wa Marekani mjini Freetown baada ya wanajeshi kuzingira nyumba yake Jumamosi iliyopita baada ya yeye kufukuzwa katika chama tawala cha All People's Congress (APC). Sumana anatuhumiwa kuanzisha harakati ya upinzani ya kisiasa na kuchochea machafuko katika mkoa wa Kono. Vilevile anatuhumiwa kusema uongo kuhusu vyeti vyake vya elimu na imani yake ya Kiislamu. Katiba ya Sierra Leone inasisitiza kuwa Makamu wa Rais anafukuzwa kazi kwa kura za thuluthi mbili ya wabunge.

0 comments:
Post a Comment