Thursday, 19 March 2015

Polisi Sudan wapewa mafunzo kusimamia uchaguzi Jeshi la Polisi nchini Sudan limetangaza kuwa, askari polisi wapatao elfu sabini wameanza kupewa mafunzo maalumu kwa minajili ya kulinda usalama katika majimbo yote, wakati wa kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo. Brigedia Siddiq Abdullah Abdulqadir, afisa mwandamizi wa jeshi la polisi la Sudan amesema kuwa, licha ya askari polisi, wanajeshi, vyombo vya usalama na taasisi za kiraia nazo zitashirikishwa katika kusimamia mwenendo mzima wa uchaguzi wa rais na bunge nchini humo. Brigedia Abdulqadir ameongeza kuwa, askari polisi hao watakuwa na jukumu la kulinda usalama wa majimbo, usalama wa wagombea wa nafasi za urais na ubunge pamoja na vituo vya kupigia kura. Wakati huohuo, Hussein Yassin Hamad, Gavana wa Jimbo la Blue Nile amesisitiza kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika katika tarehe iliyopangwa. Gavana wa Blue Nile amevitaka vyama vyote vya siasa na wananchi wa Sudan kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba ya nchi. Uchaguzi wa rais na bunge nchini Sudan umepangwa kufanyika tarehe 13 ya mwezi ujao wa Aprili.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS