Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifo wafuasi 22 wa rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, Muhammad Morsi.

Chombo kimoja cha mahakama ya Misri kimesema kuwa hukumu hiyo imetolewa kuhusiana na shambulizi lililofanywa dhidi ya kituo cha polisi katika mji wa Kerdasa nje kidogo ya jiji la Cairo ambalo lilisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi. Shambulizi hilo lilifanyika tarehe 3 Julai mwaka 2013, wakati mkuu wa majeshi ya Misri wakati huo Jenerali Abdul Fattah al Sisi ambaye ndiye Rais wa sasa wa nchi hiyo alipotangaza mapinduzi dhidi ya Muhammad Morsi.
Wafuasi wa Morsi anayeshikiliwa korokoroni, wamekuwa wakiandamwa na vyombo vya usalama na mahakama za Misri tangu baada ya kuondolewa madaraka mwezi Julai mwaka 2013. Hadi sasa mamia ya wafuasi wa Morsi na chama cha Ikhwanul Muslimin wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini Misri ambayo inakosolewa sana na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu.

0 comments:
Post a Comment