Tuesday, 17 March 2015

Steven Warren msemaji wa Pentagon amesema kuwa hata hivyo hawawezi kuthibitisha habari hiyo kuhusu Daesh kutumia gesi ya krolin
Pentagon yatiwa wasiwasi na gesi ya sumu ya Daesh
Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imeeleza wasiwasi kuhusu habari iliyotangazwa kwamba, kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limetumia gesi ya krolini. Steven Warren msemaji wa Pentagon amesema kuwa hata hivyo hawawezi kuthibitisha habari hiyo kuhusu Daesh kutumia gesi ya krolini. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani amesema kuwa utumiaji wa silaha kama gesi hiyo ya krolini ni mfano wa vitendo vya ukatili vya Daesh na ushahidi unaonyesha kuwa kundi hili limepoteza matumaini kutokana na mashinikizo yanayozidi kuliandamana. Maafisa wa eneo la Kurdistan huko Iraq Jumamosi hii walitangaza kuwa wana ushahidi usio na shaka kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limetumia mabomu yenye gesi ya krolini dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi wa Pishmerga. Baraza la Usalama lal Umoja wa Mataifa pia tarehe Sita mwezi huu lilipasisha azimio na kulaani utumiaji wa gesi ya krolini kama moja ya silaha za kemikali katika machafuko yanayoendelea huko Syria. Serikali ya Syria imeliomba mara kadhaa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liunde kamati ya kuchunguza ukweli ili kuzitambua pande zilizotumia gesi za kemikali huko Syria, hata hivyo Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimepinga ombi hilo la Syria.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS