Tuesday, 17 March 2015

Chama tawala nchini Nigeria cha PDP kimemkosoa Attahiru Jega
Mkuu wa tume ya uchaguzi Nigeria asema hatojiuzulu
Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Nigeria amesema kuwa hatojiuzulu na amepinga mwito wa baadhi ya wafuasi wa Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo waliomtaka ajiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu.

Chama tawala nchini Nigeria cha PDP kimemkosoa Attahiru Jega kuhusu namna anavyosimamia mchakato wa uchaguzi huku baadhi wakimtuhumu mkuu huyo wa tume ya uchaguzi ya Nigeria kwa kumpendelea Muhammad Buhari mtawala wa zamani wa kijeshi wa nchi hiyo ambaye ni mgombea wa kiti cha urais wa chama cha upinzani cha APC, tuhuma ambazo amezipinga.
Baadhi ya wafuasi wa Jonathan wametuma matangazo magazetini wakimtuhumu mkuu wa tume ya uchaguzi ya Nigeria kuwa anaitumbukiza nchi katika mgogoro kwa kushindwa kutengeneza na kugawa kwa wakati kadi za kupigia kura.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS