Thursday, 8 January 2015

Kamanda wa LRA akabidhiwa kwa serikali ya UgandaWaziri wa Ulinzi wa Uganda amesema kuwa, wanajeshi wa Marekani walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati wamemkabidhi  kwa vikosi vya serikali ya Uganda vilivyoko nchini humo Meja Jenerali Dominic Ongwen mmoja kati ya makamanda wa ngazi za juu wa kundi la waasi wa Lord's Resistance  Army LRA wa nchini Uganda. Dakta Chrispus Walter Kiyonga amesema kuwa, Kamanda Ongwen anayetafutwa kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, anakabiliwa na tuhuma za kutenda jinai za kivita. Hata hivyo, Waziri wa Ulinzi wa Uganda hakubainisha wazi iwapo Meja Jenerali Dominic Ongwen atafunguliwa mashtaka nchini Uganda au atapelekwa Hague, nchini Uholanzi makao makuu ya ICC. Kundi la waasi wa LRA linaloongozwa na Joseph Kony kwa zaidi ya muongo mmoja sasa limekuwa likitenda jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu nchini Uganda na hata nje ya mipaka ya nchi hiyo, na kuleta hali ya hofu na wasiwasi katika mipaka ya nchi za Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wakati hayo yakijiri, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeeleza kuwa, kutiwa mbaroni Kamanda Ongwen ni fursa nzuri ya kutekelezwa misingi ya haki za binadamu dhidi ya jinai zinazofanywa na waasi wa LRA. Shirika hilo limetaka kamanda huyo afunguliwe mashtaka haraka iwezekanavyo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS