Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya
Jinai ICC wameitaka serikali ya Ivory Coast imkabidhi kwenye korti hiyo
Simone Gbagbo, mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo, ili akashtakiwe
kutokana na tuhuma zinazomkabili.
Mwanamama huyo aliyekuwa anashikiliwa
nyumbani juzi alihamishiwa mjini Abdjan kwa ajili ya kusikilizwa kesi
yake nchini humo. Ivory Coast imekataa kumkabidhi na kusema kuwa
itamhukumu nyumbani.
Tayari rais wa zamani wa nchi hiyo
Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude mtu wa karibu wa Gbagbo
wameshafikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC mjini The
Hague Uholanzi. Watatu hao wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano
ya ndani nchini Ivory Coast yaliyopelekea watu 3,000 kuuawa, baada ya
uchaguzi wa rais wa mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment