Monday, 10 November 2014

UN: Serikali ya Burundi izungumze na wapinzani

Umoja wa Mataifa umetaka kutayarishwa anga nzuri ya kufanyika mazungumzo kati ya wanasiasa, vyama vya kisiasa na viongozi wa serikali ya Burundi.
Mshauri Maalumu wa Umoja wa Maaifa anayeshughulikia masuala ya kuzuia mauaji ya kizazi Adama Dieng ameeleza kuwa, kuna ulazima wa kufanyika mazungumzo kati ya serikali, vyama na wanasiasa kwa lengo la kuzuia kujitokeza ghasia na machafuko nchini Burundi. Dieng ameitaka serikali ya Burundi kuheshimu uhuru wa kujieleza na kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika mazungumzo kati ya serikali na vyama vya kisiasa. Mshauri Maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, wananchi wa Burundi wana haki ya kupiga kura wakiwa katika mazingira ya amani.
Uchaguzi mkuu nchini Burundi umepangwa kufanyika mwezi Juni mwakani.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS