Kamati ya pamoja ya kisiasa na kiusalama ya Sudan na Sudan Kusini imetangaza kwamba, Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na mwenzake Salva Kiir wa Sudan Kusini watakutana wiki hii kwa minajili ya kujadili kwa kina masuala ya kiusalama na mashirikiano ya pande hizo mbili. Duru za habari kutoka Khartoum zinasema kuwa, viongozi hao watajadili suala la kuainishwa mpaka wa pamoja, kutangaza eneo linalopaswa kutokuwa na silaha na vilevile kuwaondoa wanamgambo wanaobeba silaha katika eneo hilo. Wakuu wa nchi za Sudan na Sudan Kusini watajadiliana kwa kina pia suala la kuimarishwa usalama na kufunguliwa vivuko kwenye mpaka wa nchi hizo mbili. Imeelezwa kuwa, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini siku ya Alhamisi ataelekea Khartoum kwa minajili ya kukutana na Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan. Inafaa kuashiria hapa kuwa, licha ya pande hizo mbili kutiliana saini utekelezwaji wa makubaliano ya mashirikiano ya pande mbili mwezi Machi mwaka jana, amma bado zinahitilafiana kuhusiana na umiliki wa eneo Abyei, ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta.
Sunday, 12 October 2014

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment