Sunday, 12 October 2014

Israel  inataka kumfunga Spika wa Bunge la Palestina
 Mbunge wa Bunge la Palestina amesema kuwa, Mwendesha Mashtaka wa utawala wa Kizayuni wa Israel anapanga njama za kutaka itolewe hukumu ya kifungo cha miezi 38 dhidi ya Spika wa Bunge la Palestina. Khalil Rabi'i ambaye hivi karibuni aliachiliwa huru kutoka jela za Israel amesema kuwa, Mwendesha Mashtaka wa Israel anapanga njama ili Aziz  Duek Spika wa Bunge la Palestina ahukumiwe adhabu ya kifungo cha miezi 38 jela kwa tuhuma za kutoa matamshi yanayokinzana na sera za utawala huo ghasibu. Mbunge Khalil Rabi'i ameongeza kuwa, Spika  Duek pamoja na wabunge wengine kadhaa ambao wanashikiliwa kwenye korokoro za Israel wanakabiliwa na maradhi sugu, amma utawala wa Israel unagoma kutoa huduma za matibabu na dawa kwa wawakilishi hao wa Palestina. Utawala wa Kizayuni wa Israel licha ya kukiuka kinga ya wabunge wa Bunge la Palestina na kuendeleza vitendo vya ukandamizaji dhidi ya viongozi wa Kipalestina,  unawashikilia pia wabunge 36 wakiwemo mawaziri watatu wa zamani wa Palestina.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS