Sunday, 12 October 2014

Wazazi wa wasichana waliotekwa Nigeria  waja juu
 Wazazi na familia za wasichana wasiopungua 250 wa shule ya sekondari ya bweni ambao walitekwa nyara miezi sita iliyopita na wanamgambo wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, wametaka kutosahauliwa hatima ya watoto wao. Wazazi na familia za watoto hao ambao wameunda harakati waliyoipa jina la 'Warejesheni watoto wetu' walikusanyika jana na kuitaka serikali ya Nigeria kuongeza juhudi za kuwakomboa wasichana hao. Mratibu wa harakati hiyo ameeleza kwenye mjumuiko huo  na hapa tunamnukuu:' Leo hii tunawaombeni mufanye jitihada zote za kuhakikisha watoto wetu wanarudi wakiwa salama', mwisho wa kunukuu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la Boko Haram liliwashikilia mateka wasichana wapatao 270 wa shule ya sekondari ya bweni ya Chibok iliyoko katika jimbo la Borno na hadi sasa haijajulikana hatima yao. Kundi la Boko Haram lilitoa masharti ya kuwaachia wasichana hao mkabala wa kuachiliwa huru wanamgambo na baadhi ya viongozi wa kundi hilo la kigaidi wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama vya Nigeria. Serikali ya Nigeria ilitupilia mbali takwa la kundi hilo, na kusisitiza kuendeleza operesheni za kuwakomboa wasichana hao.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS