Sunday, 12 October 2014

Kuendelea machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
 Rais wa Catherine Samba-Panza wa serikali ya Mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka nchini humo. Kabla ya hapo wanamgambo hao walimtaka ajiuzulu yeye na Baraza lake la Mawaziri.Katika mkutano huo uliofanyika siku ya Jumamosi, Rais Panza, aliwataka waasi hao wa Anti-Balaka waache kukariri madai yao ya kumtaka ajiuzulu. Viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mbali na kuonyesha kusikitishwa kwao kutokana na mfululizo wa mapigano nchini humo, wamesema kuwa, machafuko yatafikia tamati siku chache zijazo na kwamba wananchi wataanza kuishi tena maisha ya kawaida. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa bado takwimu rasmi za uharibifu wa mapigano mapya yaliyoanza siku ya Jumanne iliyopita mjini Bangui, haijatangazwa. Hata hivyo ripoti zinaonyesha kuwa kwa akali askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa huku wengine sita wakijeruhiwa. Aidha mapigano hayo hadi sasa yamepelekea kufungwa Uwanja wa Ndege na kusitishwa safari za ndege mjini Bangui. Kwengineko madereva wamefanya maandamano kulalamikia kuuawa dereva mwenzao mjini Bangui. Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yameanza upya katika hali ambayo maelfu ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwamo pia askari wa Ufaransa wako nchini humo kwa lengo la kuimarisha usalama na amani ndani ya taifa hilo. Siku kadhaa zilizopita wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walitoa taarifa rasmi ya kulaani mashambulizi dhidi ya askari hao wa Umoja wa Mataifa na kulifananisha shambulizi hilo na jinai ya kivita. Wajumbe 15 wa baraza hilo la usalama wameonyesha kusikitishwa sana na kushadidi vitendo vya ukatili hususan huko Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo, na wamewataka viongozi wa serikali kufanya uchunguzi wa haraka wa kuwabaini wahusika wa shambulizi hilo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Askari wa Ufaransa wanadai kuwa wamechukua hatua za maana za kumaliza machafuko mjini Bangui. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa, askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wanamgambo wenye silaha. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, lengo la wanamgambo hao ni kuitumbukiza tena nchi hiyo katika machafuko makubwa. Ni jambo lisiloweza kusahaulika kuwa, wahanga wakubwa wa machafuko na mauaji ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ni Waislamu ambapo nchi hiyo ilitumbukia katika machafuko

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS