Sunday, 12 October 2014

Maradhi ya kipindupindu yaua watu 72 Congo DR
 Kwa akali watu 72 wamefariki dunia baada ya kukumbwa na maradhi ya kipindupindu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Dakta Mathilde Kisungi amesema kuwa, ukosefu wa huduma za vyoo na kuoga  kwenye mito na maji yaliyotuama kumechangia kwa kiasi kikubwa kusambaa maradhi ya kipindupindu nchini humo. Naye Dakta Adalbert Ngandwe Manda Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika iliyoko kusini mashariki mwa Kongo amesema kuwa, idadi ya watu waliokumbwa na maradhi ya kipindupindu imeongezeka kwa kasi katika eneo hilo. Dakta Manda ameongeza kuwa, tokea mwezi Agosti hadi sasa, jumla ya watu wasiopungua 72  tayari wameshafariki dunia kutokana na maradhi hayo.  Hii ni katika hali ambayo, idadi ya watu waliofariki dunia katika wilaya ya Tanganyika kutokana na maradhi ya Ebola katika kipindi hichohicho ni  arubaini na tatu. Inafaa kuashiria hapa kuwa, zaidi ya watu 4,000 wameshafariki dunia kutokana na maradhi ya Ebola barani Afrika na hasa katika nchi za Guinea, Liberia, Sierra Leone, Senegal, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS