Saturday, 11 October 2014

'Wamagharibi hawawezi kuzuia mwamko wa Kiislamu'
 Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, madola ya Magharibi hayawezi kuzuia mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Dakta Ali Larijani amesema kuwa, nchi za Magharibi zinapaswa kutambua kwamba, njama zao za kuunda kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh haziwezi kusambaratisha harakati ya mwamko wa Kiislamu. Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu amebainisha kwamba harakati ya mwamko wa Kiislamu ni muhimu na kwamba ilikuwepo kati ya Umma wa Kiislamu tokea karne kadhaa zilizopita. Amesisitiza kwamba mwamko wa Kiislamu ni tunu kwa Umma wa Kiislamu na wala hauwezi kusambaratika.
Dakta Larijani ameashiria harakati za kundi la kigaidi la Daesh na kusisitiza kwamba Wamagharibi hasa Wamarekani walilisaidia kundi hilo kwa maslahi yao, lakini sasa wao wenyewe wanakabiliwa na tishio la kundi hilo la kigaidi. Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa, leo hii dola la kibeberu la Marekani, Wazayuni na kundi la kigaidi la Daesh kwa pamoja wanapanga mkakati wa kuisambaratisha harakati ya mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati. Ameongeza kuwa, leo hii wananchi wa eneo la Kobani nchini Syria wamezingirwa na magaidi wa Daesh, huku muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani ukishindwa kuchukua hatua yoyote dhidi ya magaidi hao wanaoendelea kutekeleza jinai dhidi ya binadamu.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS