Msemaji wa Bunge la Liberia amesema kuwa, bunge la nchi hiyo linapinga vikali mpango wa kuakhirishwa uchaguzi wa Baraza la Seneti kama ilivyotangazwa hivi karibuni na Rais Ellen Johnson Sirleaf wa nchi hiyo kutokana na kasi ya kusambaa homa ya Ebola nchini humo.
Isaac Red amesema kuwa, wabunge wa Liberia kwa pamoja wamepitisha muswada wa kuitishwa uchaguzi wa Bunge la Seneti kabla ya tarehe 20 Disemba mwaka huu. Msemaji wa Bunge la Liberia amesema kuwa, Rais hana mamlaka ya kuakhirisha uchaguzi bila ya kuliomba bunge la nchi hiyo. Isaac Red ameongeza kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Liberia ina fursa ya kuitisha uchaguzi huo kabla ya tarehe 20 Disemba mwaka huu. Msemaji wa Bunge la Liberia amesema kuwa, Bunge pia limekataa ombi la Rais Sirleaf la kutaka kuongezewa mamlaka zaidi nchini humo.
Rais Sirleaf alitangaza hali ya hatari na kutaka aongezewe mamlaka ili aweze kukabiliana na sheria kama vile za uhuru wa vyama, uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment