Maaskofu watatu mashuhuri huko Baitul Muqaddas (Jerusalem) Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu, wamezitaka nchi zote duniani ziunge mkono juhudi za kuanzishwa na kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina katika mipaka yake ya 1967.
Askofu Michael Sabbah, Askofu Ataullah Hanna na Askofu Munib Younan wameziandikia barua nchi kadhaa duniani hasa zile za Ulaya wakizitaka ziitambue rasmi nchi huru ya Palestina, mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas. Viongozi hao wa kidini na kiroho wametaka amani ya kudumu irejeshwe katika ardhi za Palestina. Maaskofu hao wamesema kuwa, mazungumzo kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Israel hayajafikia kwenye natija. Maaskofu hao wameeleza kuwa, Marekani ambayo inadai kuwa ni mpatanishi wa mgogoro wa pande hizo mbili, inaegemea upande wa Israel na hata kujigeuza na kuwa msemaji wa Wazayuni.
0 comments:
Post a Comment