Saturday, 11 October 2014

Rais wa Somalia aponea chupuchupu kuuawa
 Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia ameponea chupuchupu kuuawa pamoja na mawaziri wake kadhaa, baada ya kundi la kigaidi la al Shabab kuishambulia ndege iliyokuwa imewabeba wakati wa kutua katika mji wa Barawe ulioko kusini mwa nchi hiyo.
Rais Hassan Sheikh Mahmoud na baadhi ya mawaziri wa serikali yake walielekea katika mji huo kwa lengo la kukagua operesheni iliyofanywa hivi karibuni na majeshi ya Somalia yakisaidiwa na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM ya kuukomboa mji huo. Muda mfupi baada ya kutokea shambulio hilo, kundi la al Shabab lilitangaza kuhusika na shambulio hilo dhidi ya ndege iliyombeba Rais wa Somalia.
Wakati huohuo, Jeshi la Kenya limetangaza kuwa limezidisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya kundi la al Shabab. David Obonyo Msemaji wa Jeshi la Kenya amesema kuwa, wanamgambo wasiopungua 60 wa al Shabab wameuawa baada ya ndege za kivita za Kenya kushambulia maeneo ya Bula Gaduud yanayohesabiwa kuwa ngome za al Shabab kusini mwa Somalia. Msemaji wa Jeshi la Kenya amesema kuwa, hadi sasa haijajulika hatima ya raia watano wa Kenya wanaoshikiliwa na kundi la al Shabab kama wako hai au wameuawa

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS