Shirika la Kimataifa la Wahajiri IOM limetoa taarifa mpya na kusema kwamba, tokea ulipoanza mwaka huu kwa akali wahajiri haramu 4,077 wameshafariki dunia katika sehemu mbalimbali duniani. Taarifa iliyotolewa na IOM imeeleza kwamba, zaidi ya wahajiri haramu 3,000 wamefariki dunia wakati wa kuvuka bahari ya Mediterranean na kuingia barani Ulaya. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, maeneo mengine ambayo wahajiri wengi haramu wamefariki dunia ni mashariki mwa Afrika na kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.
Taarifa ya Shirika la Kimataifa la Wahajiri imeeleza kuwa, kiwango cha wahanga hao kwa mwaka huu ni maradufu ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, wahajiri wengine walipoteza maisha yao baada ya kukabiliwa na mateso au kunyanyaswa katika nchi za Australia, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na Italia.
0 comments:
Post a Comment