Thursday, 2 October 2014

Somalia yakomboa mji uliodhibitiwa na al Shabab 

Kamanda wa Jeshi la Somalia amesema kuwa, vikosi vya nchi hiyo vikishirikiana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM vimefanikiwa kuukomboa mji mmoja uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo wa al Shabab kusini mwa Somalia. Mahmoud Muhammad amesema kuwa, vikosi vya Somalia na vile vya AMISOM vimefanikiwa kuukomboa mji wa Adala ulioko kusini mwa nchi hiyo bila ya kupata upinzani wowote wa wanamgambo wa al Shabab.
Kamanda Mahmoud Muhammad ameongeza kuwa, vikosi vya usalama vimeshaanza kutekeleza majukumu yake kwa lengo la kuimarisha usalama katika mji huo. Serikali ya Somalia kwa kushirikiana na vikosi vya AMISOM kuanzia mwezi uliopita zilianza kutekeleza operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya al Shabab. Operesheni hizo za kijeshi zimwezesha kukombolewa maeneo mengi yaliyokuwa yakidhibitiwa na kundi la al Shabab.
Kikosi cha AMISOM kinachoundwa na wanajeshi 22,000 kutoka nchi sita za Kiafrika kimejizatiti nchini Somalia kwa lengo la kukabiliana na kundi la al Shabab.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS