Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameitahadharisha Marekani
na nchi nyinginezo na kuzitaka zisiingilie maandamano yanayoendelea
katika mji wa Hong Kong, na kusema kuwa maandamano hayo si halali. Wangi
Yi amesema hayo alipokutana na mwenzake wa Marekani John Kerry kabla ya
kukutana huko white House na Rais Barack Obama.
Maandamano yameendelea kushuhudiwa kwa siku 4 katika mji wa kibiashara wa Hong Kong, huku baadhi ya mashule, vituo vya biashara na mabenki yakifungwa. Maandamano hayo yalianza baada ya serikali ya China kukataa uchaguzi wa wazi wa kiongozi wa mji huo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017, na kulazimisha wapiga kura wachague kutoka katika orodha ya wagombea wawili au watatu watakaopitishwa na kamati ya uteuzi. Waandamanaji hao wameapa kuendelea na maandamano hadi pale kiongozi wa Hong Kong CY Leung atakapojiuzulu.

0 comments:
Post a Comment