Tuesday, 30 September 2014

Boko Haram 300 watiwa mbaroni nchini Cameroon
 Wizara ya Ulinzi wa Cameroon imetangaza kuwa, imewatia mbaroni kwa akali wanachama 300 wa kundi la Boko Haram wenye makao yao nchini Nigeria. Gazeti la Daily Post la nchini Nigeria limemnukuu msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Cameroon akisema kuwa, wanachama wa Boko Haram waliotiwa mbaroni nchini humo wameshakabidhi silaha zao na kwa sasa vyombo vya usalama vya nchi hiyo vinaendelea kuwasaili. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni jeshi la Cameroon lilitangaza kuwa, limemtia mbaroni kiongozi mwingine mwandamizi wa Boko Haram hali inayoonyesha kuongezeka harakati za kundi hilo nchini Cameroon. Taarifa zaidi zinasema kuwa, kuenea harakati za kundi la Boko Haram katika nchi jirani hususan Cameroon kumezua wasi wasi mkubwa katika nchi zinazopakana na Nigeria. Maelfu ya watu wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009. Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza Nigeria katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS