Tuesday, 30 September 2014

Waziri Mkuu wa CAR ataka amani irejeshwe nchini
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza juu ya kukabiliana na makundi yanayosababisha ghasia na machafuko nchini humo. Mahamat Kamoun ameongeza kuwa, serikali ya Bangui itapambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu nchini humo. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameyasema hayo baada ya kundi la Kikristo la Anti Balaka kufanya shambulio dhidi ya maeneo ya Waislamu siku ya Ijumaa iliyopita. Ameongeza kuwa, serikali itaendelea na mchakato wa kuwapokonya silaha na kuwatia mbaroni na hatimaye kuwafikisha kwenye vyombo vya mahakama wale wote wanaosababisha machafuko nchini humo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, miezi michache iliyopita, makundi hasimu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yalikubali kutia saini makubaliano ya amani huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo hata hivyo machafuko bado yanaendelea nchini humo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS