Mkuu wa Kamati ya Ujasusi na Usalama
katika Bunge la Uingereza ametaka serikali ya Qatar iwekewe vikwazo.
Sir Malcolm Rifkind amesisitiza kuwa, Uingereza na nchi nyingine za
Ulaya zinapasa kuiwekea vikwazo Qatar na nchi nyingine za Kiarabu
kutokana na uungaji mkono wao wa kifedha kwa makundi ya kigaidi. Rifkind
ameongeza kuwa, Jonathan Shaw mmoja wa majenerali wa zamani wa
Uingereza alisema hivi karibuni kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo
la Ghuba ya Uajemi zinaunda makundi ya kigaidi ndani ya nchi zao. Mkuu
wa Kamati ya Ujasusi na Usalama ya Bunge la Uingereza amesema kuwa, kuna
ulazima wa kuelezwa kinagaubaga viongozi wa Qatar kwamba, uhusiano wa
kiuchumi wa London na Doha utakatika iwapo serikali ya Qatar itaendelea
kuwaunga mkono magaidi. Sir Malcolm Rifkind amebainisha kuwa, nchini
Qatar kuna vile alivyoviita 'vituo vya hisani' ambavyo hujishughulisha
na ukusanyaji fedha kwa ajili ya makundi ya kigaidi na hata kuna baadhi
ya makundi ya kigaidi yanayopata mafunzo nchini humo.
Tuesday, 30 September 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment