Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa,
harakati hiyo inasisitiza upinzani wake dhidi ya mazungumzo ya moja kwa
moja na utawala wa Kizayuni wa Israel. Mousa Abu Marzouk amesisitiza
kwamba, Wapalestina wote wanapinga mazungumzo ya mamlaka ya ndani ya
Palestina na utawala haramu wa Israel; kwani wanatambua wazi kuwa,
mazungumzo hayo hayawezi kuwa na natija ya maana. Mussa Abu Marzouk
ambaye ni kiongozi mwandamizi wa harakati ya Hamas ya Palestina amesema
kuwa, makubaliano ya harakati yao ya Fat'h yako wazi na hayana utata.
Ameongeza kuwa, jukumu muhimu kabisa la mamlaka ya ndani ya Palestina ni
kuitisha uchaguzi na kwamba, Hamas iko tayari kushiriki katika uchaguzi
wowote ukiwemo ule wa Bunge. Mwezi Juni mwaka huu serikali ya umoja wa
kitaifa iliundwa Palestina kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini kati ya
Hamas na Fat'h Aprili 23 mwaka huu.
Tuesday, 30 September 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment