Utawala wa Kizayuni wa Israel umeanza
uchunguzi kuhusiana na vifo vya wanajeshi watatu wa utawala huo
walioamua kujiua baada ya kurejea kwenye vita kati ya utawala huo na
Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Ghaza. Polisi ya Jeshi la utawala wa
Israel imetangaza kuwa, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wanajeshi hao
walijiua kutokana na matatizo ya kiakili na kisaikolojia
yaliyosababishwa na ushiriki wao kwenye vita vya Ghaza. Taarifa zinasema
kuwa, wanajeshi hao wa Israel waliamua kujiua kwa kujifyatulia risasi
na kwamba silaha walizotumia zilipatikana zikiwa pambizoni mwa
viwiliwili vyao. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanajeshi wawili kati ya
watatu walijiua kwenye kambi ya kijeshi iliyoko karibu na mpaka wa
Ukanda wa Ghaza. Nalo gazeti la Maariv linalochapishwa huko Israel
limemnukuu mmoja kati ya maafisa wa ngazi za juu wa utawala wa Israel
katika hospitali ya wagonjwa wa akili akisema kuwa, jumla ya wanajeshi
wanane wa Israel walijiua mwaka jana. Afisa huyo mwandamizi wa jeshi
amesema kuwa, jeshi la Israel halitangazi takwimu za wanajeshi wake
wanaojiua kutokana na matatizo ya kiakili.
Tuesday, 30 September 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment