Sunday, 28 September 2014

Ghandour: Wakazi wa Darfur wajiepushe na maadui  
Makamu wa Rais wa Sudan amewataka wakazi wa eneo lililogubikwa na ghasia na machafuko la Darfur kuwa macho na njama za maadui za kuzusha mifarakano.
Ibrahim Ghandour amesema kuwa, maadui wa Sudan wanafanya njama za kuibua mifarakano na hitilafu kati ya wakaazi wa eneo la Darfur na kusisitiza kwamba, wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa macho na kuimarisha umoja na mshikamano wao kwa lengo la kuzima njama hizo za maadui.
Makamu wa Rais wa Sudan amesema kuwa, chimbuko la ghasia na machafuko katika eneo hilo ni uungaji mkono wa baadhi ya madola ya kigeni kwa vibaraka wao na kusisitiza kwamba baadhi ya mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi yanafanya njama za kuzusha mapigano ya kikabila na kikoo katika eneo hilo, ili yaweze kufikia malengo yao machafu. Makamu wa Rais wa Sudan ameyataka makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha katika eneo hilo kuweka chini silaha zao na kuketi kwenye mazungumzo ya amani na serikali ya Khartoum.
Eneo la Darfur lililoko magharibi mwa Sudan linajumuisha majimbo matano na tokea mwaka 2003 hadi sasa linasumbuliwa na mapigano kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS