Monday, 10 November 2014

Polisi yachunguza tuhuma za ufisadi dhidi ya Zuma

Polisi nchini Afrika Kusini imesema inachunguza tuhuma za ufisadi dhidi ya Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.
Taarifa ya polisi kwa Bunge imekiri kwamba uchunguzi huo umeanzishwa na unajikita zaidi katika madai kwamba, Rais Zuma alitumia takriban dola milioni 24 kwa ajili ya kukarabati nyumba yake ya kibinafsi katika eneo la Nkandia. Fedha hizo zinazodaiwa kuwa mali ya umma zinasemekana zimetumika kujenga vitu vya anasa na starehe nyumbani kwa Rais Zuma kama vile ukumbi wa densi na bwawa la kuogelea.
Tayari upinzani umemtaka kiongozi huyo ajiuzulu kufuatia kashfa hiyo. Hata hivyo Rais Zuma amesema hakufahamishwa kuhusu marekebisho hayo kwenye nyumba yake. Waliosimamia shughuli hiyo wamesema vitu vilivyoongezwa kwenye nyumba ya Zuma vinahusiana na usalama kama inavyotakiwa kisheria na hakuna fedha za umma zilizofujwa.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS