Watu 70 wakiwemo wanasiasa mashuhuri wamekabidhi fomu zao kwa
Kamati Kuu ya Uchaguzi ya Tunisia kwa ajili ya kugombea kiti cha rais wa
nchi hiyo. Huo utakuwa uchaguzi wa pili wa rais nchini Tunisia baada ya
kung'olewa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Zainul Abidin bin
Ali.
Katika majina ya waliojiandikisha kwa ajili ya kiti cha raia wa Tunisia wamo baadhi ya mawaziri na maafisa wa utawala wa zamani wa nchi hiyo. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tunisia kushuhudiwa idadi kubwa kama hiyo ya watu waliojiandikisha kugombea kiti cha rais.
Sheria za uchaguzi za Tunisia zinamlazimisha mgombea yeyote wa kiti cha rais kuungwa mkono na watu wasiopungua elfu kumi au wabunge 10. Duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais wa Tunisia itafanyika tarehe 23 Novemba na iwapo hatapatikana mshindi duru ya pili ya uchaguzi huo imepangwa kufanyika tarehe 28 Disemba. Uchaguzi wa Bunge wa Tunisia pia utafanyika tarehe 26 Oktoba.

0 comments:
Post a Comment