Wednesday, 24 September 2014

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya Kiarabu na Kiafrika ametoa radiamali yake kuhusu mashambulizi yanayofanywa na Marekani nchini Syria na kusema kuwa vita dhidi ya ugaidi si mchezo wa kihollywoodi.
Hossein Amir-Abdollahian amesema kwa mtazamo wa Tehran mashambulizi yoyote ya kijeshi nchini Syria bila ya ruhusu ya nchi hiyo na pasina na kuzingatiwa sheria za kimataifa hayawezi kukubalika kwa sababu suala la kupambana na ugaidi haliwezi kuwa msingi wa kukiuka mamlaka ya kujitawala ya nchi mbalimbali.
Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa makini mashambulizi ya anga ya Marekani huko Syria na kwamba hatua hiyo ya Washington na nchi nyingine kadhaa inakiuka sheria za kimataifa na kuhalalisha uingiliaji wa nchi hizo katika masuala ya ndani ya nchi za Mashariki ya Kati. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa uingiliaji huo wa Marekani ni miongoni mwa sababu za kushadidi ugaidi na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbali na kusisitiza juu ya udharura wa kupambana na ugaidi, lakini pia inatilia mkazo umuhimu wa kulindwa sheria za kimataifa na haki za mataifa mbalimbali katika uwanja huo.
Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani mapema leo katika maeneo mbalimbali ya Syria yameua makumi ya watu wakiwemo wanawake na watoto wadogo.
KAMANDA NAE AONGEZEA KWA KUSEMA
Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Ahmad-Reza Pourdastan amesema kuwa jeshi hilo litalishambulia kundi la kitakfiri la Daesh hadi ndani ya Iraq, iwapo litajaribu kukaribia mipaka ya Iran. Brigedia Jenerali Pourdastan ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Tehran na kuongeza kuwa, hii leo jeshi la nchi kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina uwezo mkubwa wa kiulinzi hasa katika mipaka ya taifa hili. Amesema kuwa, jeshi la Iran linafuatilia kwa karibu mno matukio ya ndani ya Iraq na kwamba lipo tayari kwa ajili ya kufanya hujuma hata ndani ya nchi hiyo iwapo kundi la Daesh litakaribia mipaka ya Iran. Amesisitiza kuwa, kwa sasa kundi hilo la kitakfiri sio tishio kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akiashiria nafasi ya marjaa na viongozi wa juu wa kidini katika kuimarisha umoja wa kitaifa na kukabiliana na maadui amesema kuwa, wakati kundi la Daesh ilipokuwa tishio dhidi ya Wairaq, viongozi hao wa Kiislamu walisimama na kuwataka raia wa nchi hiyo kulinda umoja wao na kukabiliana na maadui hao.

Related Posts:


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu