Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon amesema kuwa Marekani
haina ustahiki wa kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi.
Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo kupitia hotuba aliyoitoa jana
usiku. Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria juhudi zinazodaiwa
kufanywa na Marekani kwa ajili ya kuasisi muungano dhidi ya Daesh na
kusisitiza kwamba Hizbullah inalipinga kundi la Daesh na mirengo yote ya
kitakfiri na yenye kushupalia vita na kwamba harakati hiyo inapambana
na makundi hayo. Amesema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon iko
tayari kuendesha mapambano dhidi ya makundi ambayo yanaua wananchi na
kuwatishia raia na mataifa ya eneo hili. Sayyid Hassan Nasrullah
aliongeza kama ninavyomnukuu" msimamo wetu kuhusiana na muungano wa
kimataifa hauna uhusiano wowote na msimamo wetu kuhusiana na Daesh,
kimsingi sisi tunapinga muungano wa kimataifa amma uwe dhidi ya Syria au
dhidi ya Daesh au kinyume chake; na msimamo wetu haubadiliki kuhusiana
na suala hilo na hatutakubali Lebanon iwe sehemu ya muungano huo wa
kimataifa". Mwisho wa kunukuu. Nasrulllah amekumbusha kuwa Marekani ni
chanzo kikuu cha ugaidi na muungaji mkono wa suala hilo na muungaji
mkono pia wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Amesema Marekani ilikuwa na
nafasi kuu katika kuasisiwa makundi ya kigaidi na haina ustahiki wa
kiakhlaqi wa kuendesha mapambano dhidi ya ugaidi. Katibu Mkuu wa chama
cha Hizbullah cha Lebanon amesisitiza kuwa, kama alivyosema mara kadhaa
Rais wa Marekani Barack Obama kwamba muungano huo ni kwa ajili ya
kulinda maslahi ya Marekani, hivyo wao hawana maslahi yoyote na muungano
huo.
Wednesday, 24 September 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment