Wednesday, 24 September 2014

Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya umeeleza kusikitishwa na harakati za makundi ya kitakfiri na ya kigaidi ya kuchafua jina na sura ya Uislamu.
Taarifa iliyotolewa leo na muungano huo imeashiria ukatili na mauaji yanayofanywa na makundi ya kitakfiri kama Daesh katika nchi za Iraq na Syria na kusema vitendo hivyo vinakinzana na mafundisho ya dini na vinakiuka thamani za kibinadamu.
Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Barani Ulaya umelaani vikali mauaji yanayofanywa na kundi la kitakfiti la Daesh dhidi ya wananchi wasio na hatia, wapinzani wa kisiasa na kidini na hata waandishi habari. Taarifa ya muungano huo imekosoa njama za makundi hayo ya kitakfiri za kuchafua sura ya Uislamu na kusisitiza kuwa, Waislamu barani Ulaya na duniani kote wanachukizwa mno na jinai hizo na kuzihusisha na dini ya Uislamu.

Related Posts:


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu