Wednesday, 24 September 2014

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) Nabil al Arabi amekosoa undumakuwili wa madola ya Magharibi katika kadhia ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kufumbia macho silaha za maangamizi za utawala haramu wa Israel.
Al-Arabi pia amezikosoa nchi za Kimagharibi ikiwemo Marekani kwa kuitaja mirandi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani kuwa ni hatari na wakati huo huo zinafumbia macho silaha hatari za nyuklia za utawala haramu wa Israel. Amesisitiza kuwa, kadhia ya Palestina ndio suala muhimu katika ulimwengu wa leo na kwamba, utawala wa Kizayuni unaendelea kukiuka sheria na maazimio yote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesema kuwa, Arab League imeazimia kuwasilisha pendekezo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuainisha muda wa kukomeshwa kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina.
Vilevile Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesisitizia juu ya udharura wa kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ambalo linatishia usalama wa eneo la Mashariki.

Related Posts:


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu