Bunge la Libya limeliidhinisha
baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo
Abdullah al Thani baada ya kulikataa lile la awali aliloliteuwa wiki
iliyopita. Baraza jipya la mawaziri la Libya lililoidhinishwa jana na
bunge linawajumuisha mawaziri 13 na Manaibu Waziri Mkuu watatu. Wabunge
wa Libya walilikataa baraza la mawaziri la awali lililokuwa na mawaziri
18 na kumtaka Waziri Mkuu Abdullah al Thani ateuwe timu ya mawaziri
wachache.
Abdullah al Thani ambaye alikuwa
akikaimu nafasi ya Waziri Mkuu wa Libya tangu mwezi Machi mwaka huu,
alijiuzulu baada ya uchaguzi wa mwezi Juni; na mwanzoni mwa mwezi huu
bunge jipya la Libya lilimteuwa tena kushika nafasi hiyo. Weledi wa
mambo wanasema kuwa al Thani hata hivyo ameshindwa kurejesha utulivu
huko Libya, nchi ambayo imekuwa ikikabiliwa na machafuko kwa karibu
miaka mitatu sasa baada ya kuanguka utawala wa kiongozi wa zamani wa
nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
0 comments:
Post a Comment