Tuesday, 23 September 2014

Kundi la waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati limewateka nyara raia tisa wa Cameroon kwa shabaha ya kuishinikiza serikali ya nchi hiyo imuachilie huru kiongozi wa waasi hao aliyeko jela nchini Cameroon. Gazeti la Mutations linalochapishwa Cameroon limeandika kuwa, waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wametishia kwamba, iwapo serikali ya Cameroon haitamuachilia huru Abdallah Miskin katika kipindi cha masaa 72, wataanzisha mashambulizi makali ndani ya ardhi ya Cameroon. Abdallah Miskin ni mmoja wa viongozi wa matawi ya harakati ya Seleka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Abdallah Miskin alitiwa mbaroni na kufungwa jela mwaka jana nchini Cameroon, baada ya kushadidi mapigano kati ya wanamgambo wa Seleka na kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka. Mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati umepatiwa ufumbuzi, baada ya makundi hasimu nchini humo kufikia makubaliano ya amani yaliyosainiwa miezi michache iliyopita huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS