Tuesday, 23 September 2014

Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran ina shaka na nia ya Marekani ya
Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran ina shaka na nia ya Marekani ya kutaka kupambana na ugaidi. Akizungumza na ujumbe wa maseneta kutoka nchini Kenya ulioko nchini, Hussein Amir Abdulahiyan amesema kuwa, mara baada ya kuanza mgogoro wa Syria, Iran ilizitahadharisha nchi za Magharibi juu ya matokeo mabaya na hatari ya kuyaunga mkono  makundi ya kigaidi. Abdulahiyan ameongeza kuwa, baada ya kupita muongo mmoja makundi yanayofungamana na al Qaeda yamekuwa na uzoefu mkubwa katika kutekeleza operesheni zao za kigaidi katika nchi za Afghanistan na Iraq. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, uhusiano wa Tehran na Nairobi uko katika kiwango kizuri, na kusisitiza kwamba nafasi ya mabunge na hasa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ina nafasi muhimu mno. Kwenye mazungumzo hayo, Muhammad Yussuf Haji, Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Seneti la Kenya ameelezea azma ya serikali ya nchi yake ya kuimarisha mashirikiano na Iran na kusisitiza kwamba Nairobi ina taarifa za kutosha kuhusu hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa na Iran katika nyanja za elimu na teknolojia. Haji ameongeza kuwa, Kenya inataka mashirikiano ya pande mbili katika nyanja mbalimbali yaimarishwe zaidi.kutaka kupambana na ugaidi. Akizungumza na ujumbe wa maseneta kutoka nchini Kenya ulioko nchini, Hussein Amir Abdulahiyan amesema kuwa, mara baada ya kuanza mgogoro wa Syria, Iran ilizitahadharisha nchi za Magharibi juu ya matokeo mabaya na hatari ya kuyaunga mkono  makundi ya kigaidi. Abdulahiyan ameongeza kuwa, baada ya kupita muongo mmoja makundi yanayofungamana na al Qaeda yamekuwa na uzoefu mkubwa katika kutekeleza operesheni zao za kigaidi katika nchi za Afghanistan na Iraq. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, uhusiano wa Tehran na Nairobi uko katika kiwango kizuri, na kusisitiza kwamba nafasi ya mabunge na hasa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ina nafasi muhimu mno. Kwenye mazungumzo hayo, Muhammad Yussuf Haji, Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Seneti la Kenya ameelezea azma ya serikali ya nchi yake ya kuimarisha mashirikiano na Iran na kusisitiza kwamba Nairobi ina taarifa za kutosha kuhusu hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa na Iran katika nyanja za elimu na teknolojia. Haji ameongeza kuwa, Kenya inataka mashirikiano ya pande mbili katika nyanja mbalimbali yaimarishwe zaidi.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS