Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, ugonjwa wa
ebola ambao unaendelea kusambaa kwa kasi katika eneo la magharibi mwa
Afrika, umeweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa nchini Kongo. Augustin
Matata Ponyo amesema kuwa, katika siku za hivi karibuni hakujashuhudiwa
kesi yoyote inayohusiana na maradhi ya ebola nchini humo. Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, idadi ya watu waliopatwa
na maradhi hayo kuanzia mwezi uliopita hadi sasa ni 68, na wengine 41
wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Inafaa kuashiria hapa kuwa,
kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO, zaidi ya watu
2,700 wameshafariki dunia hususan katika nchi za Liberia, Guinea na
Sierra Leone kutokana na maradhi ya ebola.
Tuesday, 23 September 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment