Tuesday, 23 September 2014

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen amesema kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo vimesambaratika kikamilifu. Akizungumza mjini Sana'a, Jamal bin Omar amesisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vya Yemen vimesambaratika na hata katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo hakuna usalama kabisa na maeneo mengine yanadhibitiwa kikamilifu na makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha.
Wakati huohuo, Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza kuwa, kwa akali watu 200 wameuawa na wengine 461 kujeruhiwa baada ya kujiri mapigano hivi karibuni mjini Sana'a kati ya wanaharakati wa al Houthi na wafuasi wa chama cha al Islaah, kinachoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, usalama umeshaanza kurejea tena kwa kiwango fulani nchini Yemen, baada ya kutiwa saini makubaliano ya kisiasa na ya amani kati ya Rais wa Yemen na harakati ya al Houthi.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS