Tuesday, 23 September 2014

Duru za Habari zimefichua kuwa, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas, katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akishinikizwa na Marekani akubali kuanza tena mazungumzo eti ya amani na utawala haramu wa Israel. Habari zinasema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, amemtaka Mahmoud Abbas kuunda mara moja timu mpya kwa ajili ya duru nyingine ya mazungumzo na Israel. Imeripotiwa kuwa, Kerry anashinikiza mazungumzo mapya kuanza mwezi ujao wa Oktoba kati ya ujumbe wa Palestina na ule wa Wazayuni. Pia kuna mpango wa kuwakutanisha tena Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala bandia wa Israel, Mahmoud Abbas na Rais Barack Obama wa Marekani huko Washington baadaye mwaka huu.
Tangu kuanza mazungumko kati ya Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina mwaka 1991, Wazayuni wamekuwa wakivuta wakati na kuendelea kupora ardhi za Wapalestina na kwa njia hiyo, mazungumzo hayo yameshindwa kufikia natija yoyote. Makundi ya wanamapambano wa Palestina yamekuwa yakisisitiza mara kwa mara kuwa, mazungumzo na Wazayuni hayana manufaa yoyote kwa Wapalestina na njia pekee ya kupata haki ni kupitia mapambano ya silaha dhidi ya utawala huo ghasibu.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS