Wednesday, 24 September 2014

Nchi kadhaa za Kiarabu zimependekeza rasimu ya azimio dhidi ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel katika mkutano wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Utangulizi huo wa azimio linaloungwa mkono na nchi 18 za Kiarabu, umeelezea wasiwasi mkubwa juu ya uwezo wa nyuklia wa utawala wa Kizayuni na kuitaka Israel ijiunge na Mkataba wa Kuzuia Kuzalisha na Kusambaza Silaha za Nyuklia (NPT).
Israel ambayo ndio utawala pekee wenye kuhodhi silaha za nyuklia katika  Mashariki ya Kati, inaripotiwa kuwa na vichwa kati ya 200 hadi 400 vya mabomu ya nyuklia.  Zaidi ya hayo, Israel haijawahi kuruhusu kukaguliwa viwanda vyake vya nyuklia na inaendelea kupuuza wito wa kimataifa wa kujiunga na mkataba wa NPT.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS